The House of Favourite Newspapers

Yanga Waipigia Bonge la Tizi Singida United

0
Wachezaji wa  Yanga wakiendelea na mazoezi  Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam  kujiandaa na mechi dhidi ya Singida United.
Nadir Haroub ‘Cannavaro’ akiwa mazoezini.
Mazoezi yakiendelea.
Ibrahim Ajibu akijifua.
Kocha mkuu wa timu hiyo Mzambia, George Lwandamina, aki wa na wachezaji wake.

BAADA ya kufanya mazoezi ya gym jana, Yanga leo imeanza mazoezi ya uwanjani kwa ajili ya kujiandaa na mechi dhidi ya Singida United.  Timu hizo, zinatarajiwa kuvaana Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Namfua mkoani Singida katika mechi ya Ligi Kuu Bara.

Chini ya kocha mkuu, Mzambia, George Lwandamina, Yanga ilikuwa ikijiandaa kwa mbinu mbalimbali.  Katika mazoezi hiyo, walikosekana wachezaji majeruhi ambao ni Mrundi Amissi Tambwe na Wazimbabwe Thabani Kamusoko na Donald Ngoma.

Akizungumzia maandalizi hayo, meneja mkuu wa timu hiyo, Hafidh Saleh,  alisema maandalizi ya kikosi hicho kwa ajili ya mchezo dhidi ya Singida yanakwenda vizuri  kuhakikisha wanapata pointi tatu muhimu.

“Kama unavyoona mwenyewe katika mazoezi haya, wachezaji watatu pekee ndiyo hawapo mazoezi kutokana na majeraha, hao  ni Tambwe, Kamusoko ambao huenda wakaikosa mechi hii.  Lakini wachezaji wengine wote wapo fiti na timu inatarajiwa kusafiri kuelekea Singida kesho kutwa Alhamisi,” alisema Saleh.

PICHA: MUSA MATEJA | GPL

Leave A Reply