The House of Favourite Newspapers

Yanga wakwea pipa na kikosi cha maangamizi

0

IMG_4230

IMG_4275

IMG_4285

IMG_4299

Mohammed Mdose,

  Dar es Salaam
KIKOSI cha Yanga, alfajiri ya leo Jumatatu kimepaa kwenda nchini Angola kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya timu ya Sagrada Esperanca ya nchini humo.

Timu hizo zinatarajiwa kukukutana keshokutwa Jumatano kwenye Uwanja wa Sagrada Esperanca mjini Dundo, Angola ambao una uwezo wa kuchukua watazamaji wapatao 8,000. Yanga imekwenda na hazina ya mabao 2-0.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, alisema kuwa wachezaji wao wote muhimu wa kikosi cha kwanza wapo kwenye msafara huo, hivyo wana matumaini makubwa ya kupata matokeo mazuri.

“Timu inaondoka na wachezaji 20 pamoja na viongozi saba, wachezaji wanaobaki ni wanne tu ambao ni Malimi Busungu, Said Juma ‘Makapu’, Issouffou Boubacar ‘Garba’ pamoja na Benedict Tinoco, hao tumewaacha kutokana na sababu mbalimbali.

“Timu itaondoka na viongozi saba ikiongozwa na mkuu wa msafara ambaye ni Ofisa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Idd Mshangama na tunatarajia kurudi Alhamisi, tunaamini tutafanya vizuri kwenye mchezo huo kwani timu imekamilika,” alisema Saleh.
Gaba na Busungu wameachwa kutokana na kuwa majeruhi huku Tinoco na Makapu wakikosa nafasi.

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave A Reply