The House of Favourite Newspapers

Ajib mambo safi Sauz

0

Ajib-mpiraIbrahim Ajib

Hans Mloli,
Dar es Salaam
MSHAMBULIAJI wa Simba, Ibrahim Ajib aliyepo nchini Afrika Kusini ‘Sauz’ akifanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa, amesema anaendelea vizuri na ana asilimia kubwa za kufaulu majaribio hayo.

Ajib ambaye alitimkia nchini humo Jumatatu ya wiki iliyopita, anaendelea kufanya majaribio kwenye kikosi cha Golden Arrows kinachoshiriki Ligi Kuu ya Sauz na mpaka sasa tayari ameshafanya kwa siku tatu mfululizo na kikosi hicho kabla ya kupumzika jana na kuendelea tena leo.

“Nashukuru Mungu kwa siku ya kwanza niliyofanya mazoezi kocha ameonyesha kunikubali, mpaka sasa nimeshafanya mazoezi kwa siku tatu na leo (jana) tumepumzika ila kesho (leo) kama kawaida,” alisema Ajib.

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave A Reply