The House of Favourite Newspapers

YANGA WALIVYOTUA DAR KUTOKEA RWANDA (PICHA +VIDEO)

TIMU ya Yanga imetua nchini jana kutokea nchini Rwanda, kukamilisha mechi zao za Kundi D ambapo wameambulia kichapo, baada ya kufungwa 1-0 na wenyeji, Rayon Sport Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali nchini.

Bao pekee la mshambuliaji Mrundi, Bonfilscaleb Bimenyimana dakika ya 19 baada ya kumzidi maarifa Nahodha wa Yanga, Kelvin Yondan na kumchambua kipa Benno Kakolanya limetosha kuwaondoa yanga kwenye mashindano ya Africa mwaka huu.

Kwa matokeo hayo, Rayon inakwenda Robo Fainali baada ya kumaliza nafasi ya pili kwa pointi zake tisa, nyuma ya USM Alger yenye pointi 11 baada ya kuifunga Gor Mahia ya Kenya leo 2-1 mjini Algiers. Yanga inamaliza nafasi ya mwisho kwa pointi zake nne, nyuma ya Gor Mahia yenye pointi nane. Mchezo mwingine wa Kundi D, USM Alger imeichapa 2-1 Gor Mahia Uwanja wa Julai 5, 1962 mjini Algiers.

PICHA: MUSA MATEJA | GPL

YANGA Walivyotua Airport Kimya Kimya

Comments are closed.