The House of Favourite Newspapers

TAARIFA MUHIMU KUTOKA OFISI YA RC MAKONDA

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam inashangazwa na taarifa zinazo sambaa mtandaoni juu ya kuwepo kwa Mkutano wa Mkuu wa Mkoa, Mh. Paul Makonda na waandishi wa habari siku ya leo tarehe 31/08/2018 katika Hoteli ya Serena muda wa saa sita mchana.

 

Taarifa hizo hazina ukweli wowote .

 

Pia Mh Makonda anasikitishwa kuwepo kwa akaunti mbalimbali za mitandao ya jamii ikiwemo Twitter, Instagram na Face book zinazotumia majina yake na kusambaza mitandaoni taarifa mbalimbali ambazo kwa namna moja au nyingine zinajenga au kumoboa na moja kwa moja kumhusisha yeye. Akaunti pekee ya mawasiliano binafsi ni akaunti ya instagram yenye jina baba_keagan na si hizo nyingine.

 

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa anaendelea na majukumu yake ya kila siku kama kawaida, anakaribisha wakazi wote waendelee kuja kupata huduma katika ofisi zake na zile za wilaya zake zote.

 

Mwisho Mkuu wa Mkoa ana kusisitiza wananchi wote kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Dr John Pombe Magufuli katika kuwaletea maendeleo watanzania wote katika nyanja zote.

Asanteni.

Imetolewa na Kitengo cha Habari,
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,
Dar es Salaaam.

 

JPM Amlipua Makonda Sakata la Makontena!

Comments are closed.