The House of Favourite Newspapers

Yanga Wankalia Pabaya Morrison

0

KLABU ya Yanga imesema haiwezi kutoa kibali cha kazi cha winga Bernard Morrison kwani ni mchezaji wao hivyo wanaishangaa Wizara ya Kazi kuwalazimisha kutoa kibali hicho.

 

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema wana mkataba na Morrison hivyo hawaoni haja ya kurudisha kibali cha kazi cha mchezaji huyo wakati bado wana kesi nae.

 

“Sisi hatujazuia ila tunacho kibali chake cha kazi. Wamekuja Wizara ya Kazi wameleta barua wakitaka turudishe kile kibali ila tumewajibu hatuwezi kurudisha kwani Morrison ni mchezaji wetu tuna mkataba naye na tuna shauri nae.

 

“Tunashangaa wameshapita makocha hapa wameondoka na hatujawahi kuulizwa na Serikali kuhusu kurudisha vibali, huwa tunarudisha wenyewe, sasa iweje kwa Morrison, ana ushawishi gani?” amesema Bumbuli.

 

Ameongeza; “Hatujazuia wala hatuna sababu ya kuzuia kwani hata Simba wametuomba uhamisho wa Morrison kwa njia ya barua na njia ya mtandao na tumewaambia kuwa huyu hatujamalizana nae.”

 

Morrison ambaye aliichezea Yanga msimu uliopita amezua utata mkubwa wa usajili baada ya hivi karibuni kusaini Simba.

Leave A Reply