The House of Favourite Newspapers

Yanga Wapangwa na Mamelodi Sundowns, Simba dhidi ya Al Ahly Robo Fainali Ligi ya Mabingwa

0

Mabingwa wa nchi Yanga wamepangwa na Mamelodi Sundowns katika hatua ya Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL.

Yanga wataanzia nyumbani katika mchezo ambao utapigwa Dimba la Benjamin Mkapa maeneo ya Temeke Jijini Dar es Salaam kati ya Machi 29,30 ama 31.

Pia Simba SC imepangwa dhidi ya Al Ahly kwenye hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye droo ya hatua hiyo inayoendelea hivi sasa mjini Cairo, Misri.

 

Leave A Reply