The House of Favourite Newspapers

Yanga Waweka Kambi kwa Maaskofu


Mwandishi Wetu | CHAMPIONI| Dar es Salaam

TIMU ya Yanga, jana iliingia kambini Baraza la Maaskofu, Kurasini jijini Dar es Salaam katika maandalizi ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika.

 

Yanga mara ya mwisho kuweka kambi mahali hapo wakati ikijiandaa na mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC ambayo ilifungwa bao 1-0.

Yanga, kesho Jumamosi inatarajiwa kujitupa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuvaana na MC Alger ya Algeria katika kuwania kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo ya kimataifa.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, timu hiyo jana jioni iliingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo mgumu.

Yanga leo (jioni) mara baada ya mazoezi, kikosi kizima tutaingia kambini kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mchezo dhidi ya MC Alger.

“Kambi hiyo tunaweka pale Baraza la Maaskofu Kurasini na lengo ni Kocha Mkuu Lwandamina (George) akae pamoja na kikosi chake katika sehemu tulivu,” alisema mtoa taarifa kutoka ndani ya Yanga.

Comments are closed.