The House of Favourite Newspapers

Amber Lulu: Bila Pombe Kali Siimbi, Siuzi Nyago!!

Amber Lulu.

 Na MWANDISHI WETU| GAZETI LA IJUMAA| STAR MIX

VIDEO Queen ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva amefungukia kazi zake kuwa bila kutumia kinywaji cha pombe kali kabla ya kuimba ama kuuza nyago kwenye video hawezi kufanya vizuri kwani atashindwa kuchetuka.

Akibonga na Ijumaa juzikati, Amber anayetikisa na Wimbo wa Watakoma alisema, mara nyingi atumiapo pombe kali humpa stimu ya kufanya kazi vizuri na pia ipo kwenye ‘damu.’

“Sijajua kwa nini yaani lakini nikitumia pombe kali huwa zinanipa stimu kinoma ya kufanya kazi zangu na bila hizo siimbi wala kushiriki freshi kwenye uandaaji wa video,” alisema Amber.

 

Comments are closed.