Yanga Yaipiga JKT Tanzania Bao 1-0, Mkwakwani, Tanga

 

BAO la Feisalum Abdalah ‘FeiToto’ dakika ya 27 akimalizia pasi ya Gadiel Michael limetosha kujibu ule usemi wa shinda mechi zako nami nishinde mechi zangu.

Walianza wapinzani wao Simba kushinda kiporo chao cha kwanza dhidi ya Mwadui kwa mabao 3-0 Uwanja wa Taifa.


Kwenye Uwanja wa Mkwakwani ambao Yanga walilazimisha sae na Coastal Union, leo wamebeba pointi tatu jumlajumla.

Matokeo hayo yanaifanya Yanga kuifunga JKT Tanzania nje ndani kwani mchezo wao wa kwanza Taifa waliifunga mabao 3-0.


Katika mchezo wa leo mashabiki walijitokeza kiduchu tofauti na ilivyokuwa mbele ya Coastal Union.

Matokeo hayo yanaifanya Yanga kufikisha pointi 58 kileleni huku wapinzani wao Simba wakiendelea kusubiri na pointi zao 38 walizonazo wakiwa nafasi ya tatu.


Pointi saba walizoziacha nyuma zimewafanya wapambane leo na kupata pointi tatu katika mchezo wao.

Yanga walianza kupoteza pointi tatu mbele ya Stand United baada ya kuchapwa bao 1-0 kisha mchezo wao dhidi ya Coastal union Uwanja wa Mkwakwani walilazimisha sare kabla ya kwenda Singida, Namfua nako wakaambulia suluhu.

Bao la Fei Toto limetosha kuikita zadi kileleni Yanga, sasa wanafikisha jumla ya pointi 58 wakiwaacha wapinzani wao Simba nafasi ya tatu wakiwa na pointi 36.

Simba wameachwa kwa jumla ya pointi 22 ili kuwafikia na kuwashusha mabingwa hao wa kihistoria nafasi ya kwanza.

Toa comment