The House of Favourite Newspapers

Yanga Yaishtukia Simba… Yasuka Mikakati Mizito Ligi Kuu Bara

0
ALI Kamwe ambaye ni Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga

ALI Kamwe ambaye ni Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, amewataka mashabiki wa timu hiyo, kuungana kwa pamoja ili kupambania vita iliyokuwepo mbele yao dhidi ya wapinzani Simba.

Kauli hiyo imekuja ikiwa ni siku chache huku timu hiyo, ikiwa inajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar.

Yanga pia hivi sasa ipo katika maandalizi ya mchezo wa hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Medeama utakaopigwa Desemba 20, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Akizungumza na Spoti Xtra, Kamwe alisema kuwa vita iliyopo dhidi ya wapinzani wao (Simba), ni  kutaka kuidhoofisha Yanga, kwa kuifananisha na timu yao baada ya kushika katika nafasi ya mwisho katika msimamo wa kundi lao la Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kamwe alisema kuwa wao Yanga wanaumizwa na pointi zao mbili walizozipata katika michezo ya kimataifa waliyoicheza.

Aliongeza kwa kuwataka mashabiki kwa pamoja kuungana kuisapoti timu yao uwanjani, ili wafanikishe malengo yao kufuzu Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika na kutetea Makombe yote ya ndani.

“Msimu huu nautabilia utakuwa mgumu, kwani tunatakiwa tufanikiwa malengo yetu ya kufika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, pamoja na kutetea Makombe yote tuliyoyachukua msimu uliopita.

“Kwani wapinzani wetu (Simba), wameonekana kuchukizwa na ubora wa kikosi chetu katika msimu huu, hiyo imekwenda mbali hadi kutaka kujifananisha na sisi katika ubora baada ya kuwa sawa mkiani katika msimamo wa makundi katika Ligi ya Mabingwa Afrika wote tukiwa na pointi mbili.

“Hii siyo vita ndogo, ni kubwa ambayo kama mashabiki hatutaungana kwa pamoja, basi hatutafikia malengo katika msimu huu,” alisema Kamwe.

#BREAKING: ISSA MBUZI WA GLOBAL TV ALAMBA SHAVU ‘FOUNTAIN GATE PRINCESS’ KUWA MRATIBU WA TIMU…

Leave A Reply