The House of Favourite Newspapers

Yanga Yaisubiri Simba Nusu Fainali Kombe la FA -Video

0

YANGA jana walifanikiwa kuonyesha kiwango cha hali ya juu kwenye mchezo wa Kombe la FA baada ya kutoka nyuma na kuwachapa Kagera Sugar mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa.

 

Hii ina maana kuwa sasa Yanga wamefufua matumaini ya Issa Liponda,Dar es Salaamkushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao ambapo sasa watatakiwa kucheza mchezo wa nusu fainali dhidi ya mshindi wa leo kati ya Simba na Azam.

Kagera Sugar ambao wapo nafasi ya nane kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara walifanikiwa kuwa wa kwanza kujipatia bao kupitia kwa kiungo wao matata Awesu Awesu katika dakika ya 19 ya mchezo, ambaye alifunga kiufundi baada ya kumhadaa kipa wa Yanga, Metacha Mnata, kuwa anapiga krosi na mpira ukajaa wavuni.

 

Kipindi cha kwanza chote Kagera walionekana kuwa bora huku wakitawala zaidi kwenye eneo la kiungo na Yanga wakipoteza mipira mingi.Mbali na bao hilo, beki wa timu hiyo David Luhende alipiga shuti kali katika dakika ya 45 baada ya kupiga shuti kali lilopaa juu ya lango la Yanga.

Nafasi pekee ambayo Yanga wanaweza kuijutia kipindi cha kwanza ni ile waliyopata dakika ya 43, ambapo kiungo wao Feisal Salum alipiga kichwa kikapaa juu.Kipindi cha pili, Yanga walionekana kuwa bora baada ya kuingia Mrisho Ngassa, ambapo katika dakika ya 51 tu alitoa pasi safi kwa mshambuliaji wa Yanga, David Molinga ambaye aliisawazishia timu yake bao safi.

 

Baada ya bao hilo, Yanga walionekana kuwa bora na kutawala mchezo lakini katika dakika ya 77 walipata penalti ambayo ilionekana kama vile Ngassa ameangushwa nje ya 18 na Juma Said Nyosso, lakini mwamuzi akaamuru ni penalti iliyofungwa na Deus Kaseke ambaye aliweka mpira huo kimiani na kuipatia Yanga bao la pili Hata hivyo, dakika chache baada ya bao hilo, Awesu Awesu alipewa kadi nyekundu ikionekana kama alijibizana vibaya na mwamuzi wa mchezo huo.

 

Katika mchezo mwingine, Wabishi wa Kusini, timu ya Namungo ilifanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali kwenye mchezo wa mapema baada ya kuichapa Alliance mabao 2-0.

 

Mabao ya Namungo yalipachikwa kimiani na Bigirimana Blaise kwa penalti na George Makang’a aliyefunga bao la kideo ndani ya 18, watavaana na Sahare au Ndanda kwenye hatua ya nusu fainali.

 

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:

⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8

⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave A Reply