The House of Favourite Newspapers

Simba SC Yachukua Kila Kitu Bara

0

UKWELI ni kwamba Simba wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2019/2020 wakiwa bora kwenye kila idara muhimu.

 

Simba wikiendi iliyopita walitangazwa kuwa mabingwa wakiwa wamefi kisha pointi 79 ambazo haziwezi kufi kiwa na timu nyingine yoyote ile, lakini wakiwa bado wamebakiza michezo sita ambayo kama wakishinda yote watazoa pointi 15 na jumla watamaliza msimu na pointi za rekodi ambazo ni 94.

Hii inaonekana kuwa rekodi kwa Simba msimu huu watakuwa wamemaliza ligi wakiwa wamedondosha pointi 17 tu msimu mzima.

 

Lakini, Simba wametwaa ubingwa huo wakionekana kuwa bora kwenye kila idara muhimu na ni sahihi kuwapa heshima makocha wa timu hiyo kutokana na kazi nzuri waliyofanya.

 

Inakuwa ngumu kwa Simba kufananishwa na timu nyingine kutokana na kuwa bora kwenye kila sehemu hadi sasa.Pamoja na kukusanya pointi hizo, timu hiyo ambayo imetwaa ubingwa mara tatu mfululizo, imefunga mabao 69 yakiwa ni 31 zaidi ya wapinzani wao Yanga ambao hadi sasa wamefunga mabao 38, pia wakiwa na mabao 29 zaidi ya Azam.

Kwa upande wa safu ya ulinzi bado wameonekana kuwa bora, Simba wameruhusu mabao 16 tu, lakini wapinzani wao Yanga wamefanikiwa kuruhusu mabao 25 na Azam wamefungwa 22.

 

Simba pia wamechukua ubingwa wakiwa wamepoteza michezo mitatu, Yanga wamepoteza minne na Azam saba, hii inaonyesha kuwa Simba walijiandaa kwa nguvu kubwa kutwaa ubingwa msimu huu.

 

Kwa upande wa takwimu za mchezaji mmoja mmoja, Simba wamefanikiwa kukaa kileleni kwenye chati ya ufungaji hadi sasa, huku staa wao Meddie Kagere akiwa na mabao 19 na pasi tano za mabao, kinara wa mabao wa Yanga ni David Molinga ambaye amefunga mabao 10 na kwa upande wa Azam ni Obrey Chirwa ambaye amefunga nane na pasi tatu.Hata hivyo pamoja na kwamba mwanzoni mwa msimu alianza kwa kusuasua, Clatous Chama anaongoza kwenye chati ya wachezaji waliopiga pasi nyingi za mabao baada ya kupiga nane na kufunga mabao mawili.

 

Staa huyo raia wa Zambia anafuatiwa na Nicolas Wadada wa Azam mwenye pasi saba za mabao na kufunga bao moja, beki wa Yanga Juma Abdul ndiye anafuata kwa kupiga pasi sita za mabao.Takwimu hizi zinaonyesha kuwa Simba walifanikiwa kujiandaa vyema kabla ya ligi na ndiyo maana mashabiki wamekuwa wakiimba: “Hata mkinuna ubingwa tumeshachukua.

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Leave A Reply