YANGA YAJIONDOA KAGAME CUP, YATUMA BARUA TFF

Mabingwa mara 27 wa Ligi Kuu Bara, Yanga imekataa mwaliko wa Chama cha Soka Afrika Mashariki (Cecafa) wa kushiriki mashindano ya Kombe la Kagame yaliyopagwa kuanza Julai 7 -21 mwaka huu nchini Rwanda.

 

Juni 2, mwaka huu, Cecafa iliwaandikia Yanga barua ya mwaliko kuhusu mashindano ya msimu huu yatakayofanyika mwezi ujao nchini Rwanda.

 

Barua ambayo imetolewa leo na idara ya habari ya Yanga kupitia msemaji wao Dismas Ten ni kwamba Yanga imejiondoa.

Katika barua hiyo ambayo imetumiwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Yanga imefikia uamuzi hayo kwa kile ilichodai wachezaji wake wengi wamemaliza mikataba.

Loading...

Toa comment