The House of Favourite Newspapers

Yanga Yachezeshwa Pira Gwaride na Tanzania Prisons

0

VINARA wa Ligi Kuu Bara, Yanga leo Desemba 31, wakiwa wanaufunga mwaka, kwenye Dimba la Nelson Mandela mjini Sumbawanga, wameshindwa kufurukuta mbele ya wajela jela Tanzania Prisons baada ya kulazimishwa sare ya 1-1, kwenye mchezo ambao uligumbikwa na rafu na matumizi makubwa ya nguvu.

 

Mchezo huo ambao umechezwa kwenye mazingira magumu baaada ya mvua kubwa kunyesha saa chache kabla ya mchezo kuanza, ulipunguza ufanisi wa timu zote mbili kwa kushindwa kuonyesha kandanda safi kutokana na maji kutuama sehemu nyingi za uwanja.

 

Tanzania Prisons walikuwa wa kwanza kumsalimia kipa Metacha Mnata, baada ya kuandika goli la kuongoza kipindi cha pili, likifungwa na Jumanne Elifadhili kwenye dakika ya 51 ya mchezo.

Baada ya goli hilo Yanga walicharuka na kuanza kulishambulia lango la wajelajela huku wakichagizwa na Deus Kaseke aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Farid Musa na kubadilisha uchezaji timu hiyo.

 

Aliyewaokoa Wananchi na Kichapo ni Saidi Ntibazonkiza alikwamisha mpira wavuni dakika ya 76, matokeo amabyo yalidumu mpaka mwisho wa mchezo.

 

Licha ya sare ya leo, Yanga bado wanaongoza ligi wakiwa na pointi 44 baada ya michezo 18, Simba nafasi ya pili na pointi 35 baada ya kucshuka dimbani mara 14 na Azam ya tatu wakiwa na pointi 32 bada ya michezo 17.

 

Leave A Reply