The House of Favourite Newspapers

Daktari Atumia Hospitali ya Serikali kwa Manufaa Binafsi

0

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima, ameagiza daktari aliyejimilikisha Hospitali ya Amana kwa lengo la kujitajirisha achukuliwe hatua kali.

 

Daktari huyo (jina kapuni) amebainika kutumia vifaa vya hospitali hiyo ambavyo vinamilikiwa na serikali  kuwatibu wagonjwa lakini malipo yote alikuwa akiyapokea binafsi.

 

Tuhuma dhidi yake zimetolewa na mgonjwa kwa wizara hiyo ambaye alilipishwa sh. laki saba na kuhudumiwa na nesi huku akiwa amelazwa gesti badala ya kulazwa kwenye wodi za wagonjwa na wala hakuambiwa anaumwa nini.

 

Gwajima ameagiza hatua zote za kinidhamu zifuatwe katika kumshughulikia daktari hiyo. Ametoa agizo hilo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Dar es Salaam alipotembelea Hospitali ya Amana kujionea utendaji kazi.

Leave A Reply