The House of Favourite Newspapers

Hali ni Shwari Ziwa Victoria, Hakuna Mauaji Wala Unyang’anyi

0

WANANCHI waishio Visiwa vilivyomo ndani ya Ziwa Victoria mkoani Mwanza wamempongeza Kamanda wa Polisi mkoani humo Murilo Jumanne kwa kuimalisha ulinzi ndani ya ziwa Victoria, ambapo awali vitendo vya uhalifu vilikuwa vimeshamili.

Wakizungumza na Global Publishers wakazi wa Kisiwa cha Juma kilichopo wilayani Sengerema mkoani Mwanza wamesema hali ya sasa ya kiusalama ndani ya Ziwa Victoria imeimalika na hakuna tena unyan’ganyi wala watu kuuwawa.

“Kipindi cha nyuma uvamizi ziwani ulikuwa ni tishio watu tulikuwa tunanyan’ganywa boti, mitumbwi na watu kuuwawa, lakini tangu Kamanda Murilo alipokuja Mwanza kwa kweli tumefarijika tuna amani maana ulinzi imeimalika,”alisema Boniphas Ncheye mkazi wa kijiji cha Karumo Mwalo wa Isingilo.

Aidha, Kamanda Murilo baada ya kufika kisiwani hapo alipokuwa akifanya doria, aliwataka wananchi kuendelea kuwafichua wale wote wanaowahifadhi wa halifu na kusababisha uvunjifu wa amani na upotevu wa mali za watu.

“Kufanya vizuri kwa jeshi la polisi ndani ya Ziwa Victoria kumetokana na ushirikiano mkubwa wa wananchi hivyo tuendelee hivyo na tusimuonee haya mtu yoyote.anaye jaribu kuvunja amani na hiki ni kipindi cha siku kuu kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake,” alisema Murilo.

Na Leah Marco, MWANZA.

Leave A Reply