The House of Favourite Newspapers

Yanga Yamgeukia Kiungo Simba

0

WASHINDWEwenyewe tu! Ndivyo unavyoweza kusema kwani tayari Yanga wametajiwa dau la kumnasa kiungo wa klabu ya Simba anayecheza kwa mkopo Polisi Tanzania, Marcel Kaheza kuwa ni Sh mil 30.

 

Kaheza ambaye mkataba wake na Simba unaisha mwishoni mwa msimu huu, amekuwa wa moto baada ya kuhusika kwenye mabao 12 ya Polisi Tanzania, akifunga mabao saba na kuasisti mara tano.Kasi yake hiyo inaonekana kuzivutia timu nyingi ikiwemo Yanga.

 

Akizungumza na Cham-pioni Jumamosi, meneja wa mchezaji huyo, Kally Ongala, alisema mazungumzo hayo yanaendelea vizuri na tayari wamekubaliana mambo machache mpaka sasa hivyo wanasubiri dirisha la usajili lifun-guliwe ili kukamili-sha dili hilo.

 

“Ni kweli Yanga wametu-fuata kwa ajili ya kuhitaji huduma ya mchezaji wetu Kaheza kwa ajili ya kujiunga nao kwa msimu ujao, na tayari tumesha-fanya mazungumzo ya awali juu ya kukamilisha dili hilo hivyo kinachosubiriwa sasa ni kufunguliwa kwa dirisha la usajili.

 

“Ukiwatoa Yanga pia tunazo ofa kutoka klabu nyingine mbili kubwa, moja ya hapa nchini na nyingine ni ya nje, hivyo tutaangalia nani ataleta dau nono ambalo halipaswi kuwa chini ya mil 30 kwa mkataba wa miaka miwili,” alisema Ongala

Leave A Reply