The House of Favourite Newspapers

Yanga Yapeleka Ofa Kwa Mrithi wa Niyonzima

0

HATIMAYE Kamati ya Usajili ya Yanga, inayoongozwa na Makamu Mwenyeikiti wake, Eng. Hersi Said, imedaiwa kufanikiwa kupenyeza ofa yao ya kumnasa kiungo mshambuliaji wa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, raia wa Kenya, Anthon Akumu ili aje kurithi mikoba ya Haruna Nyinzima.


Tangu Julai 15, mwaka huu,
baada ya Yanga kumuaga rasmi nyota Niyonzima ambaye ni raia wa Rwanda, imefahamika wazi kuingia moja kwa moja kwenye mawindo ya kupata mbadala wake, ambapo imegota kwa Athon Akumu anayeitumikia Kaizer.

Taarifa kutoka kwa mmoja wa viongozi wa timu ya Kaizer Chiefs, Vina Maphosa, ameliambia Championi Ijumaa kwamba, ni kweli amesikia taarifa za Yanga kuleta ombi wakati yeye na timu hiyo walikuwa nchini Morocco ambako walienda kwa ajili ya Fainali ya Kombe la Mabingwa Afrika.

 

“Kuhusu suala la Yanga kumhitaji Akumu, kwa sasa mimi siwezi sana kulielezea maana ndiyo nimetua muda si mrefu nikitokea Morocco, ambapo nilienda kwa ajili ya mchezo wetu na Al Ahly, hivyo nitakuwa na mapumziko kwa takriban siku tano.

 

“Zaidi nikuombe uwe mvumilivu maana nitajua hilo suala baada ya kuingia kazini kuanzia Jumatatu ya Julai 26, mwaka huu, hapo sasa nitakuwa na majibu ya wazi juu ya jambo hilo,” alisema Maphosa.

MUSA MATEJA,Dar es Salaam

Leave A Reply