The House of Favourite Newspapers

Yanga Yashika Nafasi Ya 3 Kwa Ubora Afrika, Simba Ya 12

0

Mtandao wa International Federation of Football History and Statistics (IFFHS) umetoka taarifa ya takwimu za vilabu bora Duniani kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Septemba 22 2022 hadi Agosti 21 2023.

Upande wa AFRIKA unaonyesha klabu ya YANGA ya Tanzania inashika nafasi ya 3 nyuma ya vilabu vya Ahly ya Misri na Wydad ya Morocco. Huku wababe wa Msimbazi SIMBA SC wakiangukia nafasi ya 12.

Yanga msimu uliopita ilicheza fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF na kupoteza kwa klabu ya USM ALGER ya Algeria , Mabingwa hao wa CAFCC wanashika nafasi ya 10 kwenye orodha hiyo. Mabingwa wa African Football League Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini wako nafasi ya 5 baada ya Pyramid ya Misri huku nafasi ya 6 ikienda kwa FAR RABAT, Raja CA iko nafasi ya 7, Zamalek ya Misri 8 na CR BELOUZIDAD ikiwa ya 9

Mtandao wa IFFHS umekuwa maarufu sana Tanzania kwa siku za karibuni na kujizolea sifa miongoni mwa mashabiki wa soka kwa namna wanavyoziona klabu zao zikipepea nafasi za juu kwenye takwimu zao.

10 bora Afrika ipo hivi;

1. Al Ahly
2. Wydad Casablanca
3. Yanga
4. Pyramids FC
5. Mamelodi Sundowns
6. Raja Casablanca
7. FAR Rabat
8. CR Belouizdad
9. Zamalek SC
10. Esperance

Leave A Reply