The House of Favourite Newspapers

Yanga Yashusha Kiungo, Winga wa Kulia wa KCCA FC, Moses Aliro

0
Moses Aliro

KIKOSI cha Yanga, jana kimesafairi kuelekea nchini Malawi, kikiwa na wachezaji wapya wawili wote raia wa Uganda watakaokwenda kucheza mchezo mmoja wa kirafiki.

Yanga inatarajiwa kucheza mchezo huo wa kirafiki leo Alhamisi dhidi ya Nyasa Big Bullets ambao umeandaliwa maalum katika kusherehekea Siku ya Uhuru wa Malawi.

Wachezaji hao waliokuwepo katika msafara huo ni kiungo mchezeshaji wa Klabu ya Wakiso Giants, Sharif Kimbowa na winga wa kulia wa KCCA FC, Moses Aliro.

Nyota hao wote walikuwepo katika msafara huo uliohusisha wachezaji wa kikosi cha wakubwa na vijana cha Yanga ambao ulitua jana mchana kabla ya jioni kula chakula jioni katika Ikulu ya Malawi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Kamati ya Utendaji ya Yanga, wachezaji hao wameungana na wenzao kwa ajili ya kufanyiwa majaribio watakapocheza dhidi ya Nyasa Big Bullets.

Mtoa taarifa huyo alisema Kocha Mkuu wa Timu ya Vijana, Said Maulid, atakayekuwepo katika benchi la ufundi katika mchezo huo, ndiye atakayeangalia ubora wa wachezaji hao kabla ya kusajiliwa.

Aliongeza kuwa, pia meneja wa timu hiyo, Walter Harrison na Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said waliokuwepo katika msafara huo, watashirikiana kutathimini viwango vya wachezaji hao.

“Kikosi kimeondoka nchini leo (jana) asubuhi kuelekea Malawi kikiwa na wachezaji wawili wapya raia wa Uganda ambao ni Sharif Kimbowa kutoka Klabu ya Wakiso Giants na Moses Aliro anayetokea KCCA FC.

“Wachezaji hao wawili wote wapo Yanga kwa ajili ya kufanya majaribio na endapo watamshawishi Kocha Mkuu, Gamond (Muguel), basi watapewa mikataba ya kudumu.”

STORI NA WILBERT MOLANDI

#EXCLUSIVE: CHINO AFUNGUKA ALIVYOTREND – ”MSINIGOMBANISHE na DIAMOND, HAIJANIONGEZEA CHOCHOTE”…

Leave A Reply