The House of Favourite Newspapers

Yanga Yataja Zilipo Pointi za Ubingwa

0

BEKI wa kati wa Yanga, Bakari Nondo Mwamnyeto, amefunguka kuwa watakwenda kuvuna pointi tatu mbele ya JKT Tanzania, baada ya kukosa ushindi kwenye michezo mitatu mfufulizo ya Ligi Kuu Bara.

 

Mwamnyeto alisema pointi hizo tatu ndiyo ambazo zitaenda kuongeza matumaini yao ya kumaliza ligi wakiwa mabingwa, kwani bado wanaiona nafasi ya kutwaa kombe hilo.

 

Kesho Jumatano, Yanga watapambana na JKT Tanzania kwenye mchezo ambao unatazamiwa kuwa mgumu kwa kuwa JKT Tanzania hawapo mahali salama kwenye msimamo wa ligi hiyo wakipambana kuepuka janga la kushuka daraja.

 

Wakati JKT Tanzania wakipambana kuepuka kushuka daraja, Yanga wenyewe wanausaka ubingwa baada ya kuukosa kwa misimu mitatu mfululizo sasa.

Akizungumza na Spoti Xtra, Mwamnyeto alisema: “Pointi tatu ambazo tunakwenda kuziwania kwenye mchezo wetu dhidi ya JKT ni muhimu sana kwa sababu zitakuwa zinazidi kuweka matumaini yetu ya kutwaa ubingwa msimu huu.

 

“Najua mchezo hautakuwa rahisi kwa sababu JKT watakuwa nyumbani wakipambana kuepuka janga la kushuka daraja. Lakini kwa namna ambavyo tunahitaji pointi tatu kwenye mchezo huo, naamini tutapata ushindi.

 

”Timu hizo ambazo zinakwenda kupambana Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, zilipokutana Novemba 28, mwaka jana Uwanja wa Mkapa, Dar, Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Deus Kaseke dakika ya 33 akimalizia pasi ya Yacouba Songne.

STORI NA ISSA LIPONDA

Leave A Reply