Yanga Yatamba Kuwanyoosha AS Vita

Kikosi cha timu ya Yanga.

KUELEKEA kwenye kilele cha siku ya Wananchi, uongozi wa Yanga umesema kuwa utawapiga mabao mengi AS Vita kwenye mchezo wa kirafiki utakaochezwa Uwanja wa Taifa.

 

Yanga itamenyana na AS Vita Agosti 4 wakiongozwa na kauli mbiu ya ‘Tunakusanya Kijiji’ na mchakato unaanza Julai 28.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema; “Usajili wetu msimu huu ni wa uhakika na tuna imani ya kufanya makubwa zaidi kitaifa na kimataifa kwa kuanza tunaanza kazi na hawa AS Vita kisha wengine watafuata.”

“Tutashusha muziki wote wa mashine zetu zote tulizonazo, kwa sasa wachezaji etu wapo kambini Morogoro wakirejea watakuwa wameiva kisawasawa hivyo hao AS Vita wasitarajie wepesi lazima watakalishwa tu,” alisema Mwakalebela ambaye ni kiongozi wa zamani wa Mtibwa na TFF.

 

Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh ameliambia Spoti Xtra kuwa morali ya wachezaji ni kubwa kambini na wanajipanga kwa michezo yote ya Ligi na ile ya kimataifa. Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Dismas Ten alisema; “Usajili wa michuano ya kimataifa ya Caf tayari tumeshamaliza kwani tulikuwa tunatambua kwamba kuna adhabu hivyo hatuna presha kwa sasa kazi imeisha.”


Loading...

Toa comment