Yanga Yatambulisha CEO Mpya Andre Matine, Wazindua App Ya Mashabiki – Video
KLABU ya Yanga, leo Septemba 27, 2022 imemtangaza Andre Matine kuwa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo kutoka klabu ya TP Mazembe ya DR Congo.
“Niliulizwa kwa nini nimeichagua Yanga, jibu langu lilikuwa ni rahisi tu, kwa sababu Yanga ni klabu kubwa Afrika,” amesema Andre Mtine, raia wa Zambia aliyetangazwa kuwa Mtendaji Mkuu (CEO) mpya wa Yanga.
“Huu ni muendelezo wa ajenda yangu kubwa katika uongozi wangu ambayo ni kuimarisha klabu kiuchumi, kupitia App na tovuti hii kunafungua mlango kwa mashabiki na wapenzi wa Young Africans SC kuweza kujisajili kuwa shabiki au mwanachama rasmi,” amesema Hersi Ally Said, Rais wa Yanga.
Pia Klabu ya Yanga leo imezindua tovuti na App rasmi ya klabu hiyo ambayo itarahisishia wanachama, mashabiki na wapenzi wao kupata taarifa na maudhui mbalimbali kuhusiana na timu yao.