The House of Favourite Newspapers

Yanga Yatangaza Hali ya Hatari Dhidi ya Namungo Ligi Kuu

0

UONGOZI wa Yanga, umeweka wazi kuwa, kikosi chao kimerejea Bongo kamili kwa ajili ya kuwavaa wapinzani wao Namungo katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa kesho Jumatano kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar.

Timu hiyo imetoka kucheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Merrikh na kupata ushindi wa mabao 0-2, ugenini.

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, amesema wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na malengo ni kupata ushindi.

“Mchezo wetu dhidi ya Al Merrikh umeisha, sasa ni kuona tunapata ushindi kwenye mchezo wetu dhidi ya Namungo ili kurejea katika kuongoza Ligi Kwa kuwa huu kwetu ni mchezo muhimu na wachezaji wapo tayari.

“Kutakuwa na kazi ya kuwapa maua mashabiki waliojitokeza Rwanda Kwa wingi na kuandika rekodi ambayo ni kubwa, hivyo wale ambao hawaja Rwanda ni muda wao kujitokeza Azam Complex, ikifika dakika ya 12 watasimama na kukutana na sapraizi, hivyo wajitokeze kwa wingi ili kuona hicho ambacho kitafanyika,” alisema Kamwe.

WAANDISHI: LUNYAMADZO MLYUKA, CHRISTINA FELICIAN, LULU MPALANZI NA LEILA SAID

KOCHA wa WAARABU AWAHOFIA YANGA/ MASHINE 4 ZAONGEZA MZUKA SIMBA SC/ SINGIDA YAJA MOTO…

Leave A Reply