The House of Favourite Newspapers

Yanga Yatinga Fainali ya Kombe la FA, Yamsubiri Azam au Coastal Union

0
Mchezaji wa Yanga Feisal Salum Fei Toto akishangilia bao pekee lililoipeleka Yanga Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam

KLABU ya Yanga imefanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam baada ya kuifunga klabu ya Simba kwa jumla ya bao 1-0 bao lililofungwa na Feisal Salum kipindi cha kwanza cha mchezo.

 

Mchezo ulikuwa na kasi huku timu zote zikifanikiwa kutengeneza nafasi za mabao lakini umakini ulikuwa mdogo kwa washambuliaji wa pande zote mbili ikiongozwa na Yanga ambayo ilicheza na washambuliaji wawili Fiston Mayele pamoja na Heritier Makambo.

Kiungo wa Yanga Salum Abubakar ‘Sure Boy’ akipiga pasi katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam kwenye Uwanja wa CCM Kirumba

Mchezo ulishuhudia majeruhi wawili Kibwana Shomari pamoja na Kibu Denis ambao walipata majeraha ya kichwa baada ya kugongana kwenye mpira wa juu.

 

Nusu fainali ya pili inatarajiwa kuchezwa kesho kati ya Azam na Coastal Union ambayo mshindi baina yao ataungana na klabu ya Yanga katika kucheza fainali ya kombe hilo la Shirikisho mkoani Arusha

 

 

Leave A Reply