The House of Favourite Newspapers

Yanga Yavitikisa Vigogo Afrika Yapanda Nafasi za Ubora Baada Kutinga Robo Fainali

0

HABARI njema kwa mashabiki wa Yanga ni timu hiyo kupanda nafasi za ubora kwa timu za Afrika mara baada ya kutinga robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga hapo awali ilikuwa nafasi mbaya zaidi kwa ubora Afrika kutokana na kushindwa kufanya vyema kwa misimu mitano mfululizo katika michuano hiyo.

Yanga mara ya mwisho kutinga katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho ilikuwa mwaka 2018 ambapo ilimaliza wa mwisho katika kundi ambalo lilikuwa na timu za MC Algers, Rayon Sports na Gor Mahia ya Kenya.

Kitendo cha kutinga robo fainali tena kwa kuwafunga Monastir kwa mabao 2-0 kimewapa nafasi ya kusonga mbele kwenye viwango vya soka Afrika.

Taarifa ambazo limezipata Gazeti la Championi Jumatano juu ya Yanga kupanda nafasi za ubora ni kutokana na pointi ambazo timu hiyo imezivuna mara baada ya kufuzu kwenda katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho.

Kabla ya kuanza kwa msimu huu wa kimataifa Yanga walikuwa wanakamata nafasi ya 75 kwa viwango vya klabu zinazoshiriki ligi ya Afrika lakini mara baada ya kufuzu kwenda robo fainali ya Shirikisho Yanga wamepanda mpaka kufikia nafasi ya 27.

Kwa maana hiyo Yanga imepanda kwa nafasi 48 jambo ambalo limetajwa na majarida makubwa Afrika kuwa Yanga ni miongoni mwa timu ambazo zimepanda kwa kiasi kukubwa kwa viwango Afrika.

Stori: Marco Mzumbe

WAZIRI UMMY ATOA TAMKO UGONJWA ULIOUA WATANO KAGERA – ”HAUNA TIBA, NI MARBURG”…

Leave A Reply