The House of Favourite Newspapers

Yanga Yawazidi Ujanja Wanigeria

0

KATIKA kuhakikisha wanapangua hujuma za wapinzani wao Rivers United ya Nigeria, Yanga juzi iliwapima mastaa wake wote corona katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Kati ya wachezaji ambao Yanga wanahofia huenda wakapewa ‘corona feki’ ili wasicheze huko Nigeria keshokutwa, ni mshambuliaji Mkongomani, Heritiel Makambo.

Yanga imeondoka jana Ijumaa ikiwa na kikosi cha wachezaji 25 na viongozi nane, pamoja na mashabiki zaidi ya 100.

Yanga inatarajiwa kuvaana na River katika mchezo wa pili wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika huku ikiwa imekalia kuti kavu kutokana na kupoteza 1-0 jijini Dar Jumapili iliyopita.

Mmoja wa mabosi wa Yanga, ameliambia Championi, kuwa lengo la kuwapima wachezaji hao Dar, ni kuhofia hujuma za wachezaji wao mastaa ‘kupewa’ corona mara baada ya kutua Nigeria.

Aliongeza kuwa wanafahamu hujuma zote ambazo wapinzani wao wamepanga kuzifanya, hiyo ndiyo sababu ya kumtanguliza Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Senzo Mazingisa nchini Nigeria kwa ajili ya kuandaa mazingira timu itakapofikia huko.

“Tunafahamu kabisa wapo baadhi ya wachezaji wanaowahofia Rivers, kati ya hao ni Makambo.

“Tumejipanga kukubaliana na hujuma zote zitakazotokea huko, hivyo tumewapima hapa nyumbani kabla ya kwenda Nigeria.

“Vipimo hivyo tumepanga kusafiri navyo kama vidhibiti mara baada ya kufika huko,” alisema bosi huyo.

Akizungumzia hilo, Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo, Frederick Mwakalebela alisema kuwa: “Tumejipanga vema katika kila idara ili kuhakikisha tunapata matokeo mazuri, mashabiki waondoe hofu.”

Leave A Reply