The House of Favourite Newspapers

Yassine Bounou Ajiunga na miamba ya Saudi Arabia Akitoka Sevilla ya Uhispania

0

Mmoja wa mashujaa wa Afrika kwenye kombe la Dunia 2022, Mmoroco Yassine Bounou almaarufu Bono amejiunga na miamba ya Saudi Arabia, klabu ya Al Hilal kwa ada ya uhamisho ya euro milioni 21 kutoka Sevilla ya Uhispania.

Bono (32) mzaliwa wa Canada mwenye uraia wa Morocco amesaini mkataba wa miaka mitatu ya kuitumikia miamba hiyo ya Saudi Arabia mpaka Juni 2026.

Bono ameichezea Sevilla ya Uhispania mechi 142 akicheza mechi 58 bila kuruhusu goli (clean sheets), ameifungia miamba hiyo ya Uhispania goli moja huku akiisaidia kutwaa makombe mawili ya EUROPA League sambamba na kuwa golikipa namba tatu kombe la Duniani 2022.

Bono amekuwa golikipa wa kwanza kwenye karne ya 21 kuwa na asilimia 50 ya clean sheets kwenye msimu mmoja ndani ya Sevilla.

Leave A Reply