The House of Favourite Newspapers

Young Dee: Masogange Alikuwa Mtu Wa Watu

Msanii wa Bongo Fleva, David Genzi maarufu kama Young Dee.

 

MUDA mfupi baada ya mwili wa Video Queen, Agnes Gerald ‘Masogange’ kuzikwa jijini Mbeya, msanii wa Bongo Fleva, David Genzi maarufu kama Young Dee, amesema marehemu alikuwa mtu wa watu.

 

Masogange alifariki dunia Ijumaa iliyopita kwenye Hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam baada ya kuugua Ugonjwa wa Nimonia na upungufu wa damu mwilini na kisha kuzikwa juzi Jumatatu.

Video Queen, Agnes Gerald ‘Masogange’.

Akizungumza na Championi Jumatano, Young Dee alisema kipindi cha uhai wake, Masogange alikuwa ni mtu wa watu ambaye alikuwa hapendi ugomvi na hajawahi kusikia akigombana na mtu japo yeye hajawahi kufanya naye kazi.

 

“Japo sijawahi kufanya naye kazi, lakini alikuwa mtu wa watu kwani sijawahi kusikia akigombana na mtu yeyote, kwa sasa wasanii tuendelee kumuomba Mungu na tuachane na maovu pia tuwe wamoja kwani hujui lini utakufa,” alisema Young Dee.

 

Young Dee kwa sasa anatamba na ngoma yake ya Kiutani Utani.

Comments are closed.