The House of Favourite Newspapers

Wolper Aitabiria Kifo Bongo Movie, Awataka Waache Unafiki

STAA wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper, amekubali kushindwa kwenye upande wa filamu na hatimaye kuamua kuwekeza nguvu zake  kwenye upande ushonaji ambao amekuwa akifanya kama sehemu yake nyingine kujiongezea kipato.

Katika kuonyesha dhamira na hisia zake, Wolper  leo ameamua kupost kwenye ukurasa wake wa Instagram ujumbe ufuatao:

”Natamani Bongo movie Tupendane saana yani saaaaana, kiukweli na syo kinafk kiasi kwamba ata mtu akitokea akamuongelea bongo movie vibaya basi wote tusimame nae paka ajute kwanini kafanya hlo tukio, lakini maskin ya Mungu mchawi wetu kafa atujui kaburi lake tukamuombe Radhi atusamehe tuwe huru..yani Mtu akikosea ndio kwanza Tunakandamiza nakuonyesha wasioliona lile kosa ichi ni kilio nanimsiba mkubwa R.i.p Bongo movie.
Acha nipambane na cherehani zangu niangalie nijinsi gani nakomboa mafundi chereani na Tuheshimike Tanzania hope Mafundi chereani amtoniangusha na amtokua wanafki 🙏.”

 

Comments are closed.