The House of Favourite Newspapers

Yupo Wapi Kamanda Kova; Sasa ni Mwalimu wa Ujasiriamali

0

NAAM mpendwa msomaji wetu wa kolamu ya Yupo Wapi ambayo imekuwa ikikuletea watu waliowahi kuwa maarufu na kisha kupotea machoni na masikioni mwa wengi ambapo leo ninakuletea aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.

Kamanda Kova amekuwa na sifa ya kudhibiti uhalifu kila kila mkoa aliopelekwa kuwa kamanda wa mkoa (RPC) ikiwemo mkoa wa Pwani, Mbeya na mingineyo kabla ya kupewa Mkoa wa Dar es Salaam ambao baadaye ukapewa hadhi ya Kanda Maalum ya Polisi.

Kamanda Kova alistaafu Desemba 31, 2015 baada ya hapo alipotea kabisa machoni na midomoni mwaka wengi lakini mwishoni mwa wiki iliyopita mwandishi wetu alikutana naye eneo la Suma JKT Mwenge jijini Dar ambapo kulikuwa na hafla ya kikundi ya Vicoba cha FATA kilikuwa kikifanya sherehe ya kuufunga mwaka.

Baada ya mwanahabari wetu kukutana na Kamanda Kova mahojiano yalianza kama ifuatavyo:

Risasi: Kamanda tangu ustaafu umepotea sana siku hizi uko wapi?

Kamanda Kova: Mimi niko hapahapa Dar napiga dili zangu kama kawaida.

 

Risasi: Uko Dar sehemu gani?

Kamanda Kova: Naishi maeneo ya Kitunda kule ukifika ukiuliza kwa Kova utafika bila shaka.

Risasi: Unajisikiaje kuiacha kazi yako uliyoizoea?

Kamanda Kova: Ukweli japo nimestaafu kazi lakini kutokana na nilivyoishi vizuri na wananchi wamekuwa wakiendelea kunishangilia na kuniita kila ninapoonekana.

 

Risasi: Vipi sasa hivi umekaa unakula mafao tu au unapiga dili gani?

Kamanda Kova: Mimi sasa hivi ni mjasiriamali na ni kiongozi wa Chama cha Wastaafu hapa nchini ambaye nina jukumu la kuwapa mafunzo wastaafu ili waishi maisha bora baada ya kustaafu na kuondokana na kuwa tegemezi baada ya kumaliza mafao.

Risasi: Wewe unafanya ujasiriamali upi?

Kamanda Kova: Mimi nafuga mifugo ya aina mbalimbali kama vile kuku, mbuzi na mifugo mingine na pia nina mashine za kutengezea vyakula vya mifugo kama vile ng’ombe, mbuzi na mifugo mingine. Pamoja na hayo nina mashine za kusaga na kukoboa nafaka ambazo nazo zinanifanya nijiimarishe kwenye ujasiriamali wangu.

 

Risasi: Unawashauri nini wastaafu wenzako?

Kamanda Kova: Nawashauri wajiimarishe katika ujasiriamali ili waweze kuishi maisha bora baada ya kustaafu.

Maoni/Ushauri | 0713 562 001

Leave A Reply