The House of Favourite Newspapers

Zahera Ajitetea Baada ya ‘Kupigwa’ na Polisi – Video

KOCHA Mkuu wa timu ya Yanga, Mwinyi Zahera, amesema tatizo la jana kufungwa mabao 2-0 na timu ya Polisi Tanzania katika mchezo wa kirafiki uliofanyika  uwanja wa  Ushirika-Moshi, lilikuwa ni uwanja huo uliowafanya wachezaji wake kushindwa kutoa pasi za uhakika.

“Tatizo la kwanza lilikuwa ni uwanja, wachezaji wengi tuliowatumia kwenye mchezo dhidi ya Polisi  Tanzania wanachezea sana mpira lakini kutokana na hali ya uwanja ilikuwa ni ngumu kuona pasi.  Mpira unapigwa tu mbele, hilo lilikuwa tatizo kwetu,” alisema kocha huyo na kuongeza:

“Kikosi ambacho kitacheza mchezo dhidi ya Township ni tofauti na ambacho kimecheza na Polisi Tanzania. Tunapowapa nafasi wachezaji kwenye mechi kama hizi wanatakiwa kuonyesha uwezo lakini kuna baadhi ya wachezaji itakuwa ngumu kucheza kikosi cha kwanza cha Yanga msimu huu.”

MSIKIE ZAHERA

Comments are closed.