The House of Favourite Newspapers

Zahera ampa Sibomana dakika 180 Yanga SC

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amepanga kuitumia michezo miwili ambayo wataicheza visiwani Zanzibar kama moja ya sehemu za kutafuta namna ya kuwadhibiti wapinzani wake Township Rollers ambao watacheza nao Jumamosi hii katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Kwa mara ya kwanza baada ya msimu uliopita Yanga kutoshiriki michuano ya kimataifa, sasa watashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo wataanzia nyumbani Jumamosi hii kuvaana na Rollers katika mechi itakayopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Zahera amesema kuwa kikosi chake bado hakijakaa sawa lakini atatumia michezo hiyo miwili ya visiwani Zanzibar ambapo wameenda tangu juzi Jumatatu kwa ajili ya kujiweka sawa na kuangalia kikosi chake kabla ya kupambana kwenye mechi hiyo na Rollers.

 

“Bado kikosi changu hakipo sawa, ilikuwa ninahitaji siku 15 zaidi ili tuwe sawa kwa sababu ya mazoezi magumu ambayo timu ilikuwa ikifanya kule Morogoro na hata siku moja tuliporudi hapa Dar kucheza na Kariobangi.

 

“Licha ya kwamba hatutakuwa sawa kama vile ambavyo mimi ninahitaji lakini nitatumia hizi mechi mbili za Zanzibar kuona kwamba nakiweka tayari kikosi ili tucheze katika mechi hiyo na Rollers japo inaweza kuwa ngumu kwa sababu bado miili ya wachezaji ina uchovu ndani yake,” alisema Zahera.

LIVE: MAGAZETI AUG 08: BOT YAONYA WANAOFANYA USHIRIKINA WA NOTI

Comments are closed.