The House of Favourite Newspapers

Zahera Atua Dar Kuwashuhudia Simba Vs Yanga

0
Mwinyi Zahera

ALIYEKUWA Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amefunguka kuwa amerejea nchini kwa ajili ya kuangalia mchezo wa timu yake ya zamani dhidi ya Simba ambao utapigwa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

 

Zahera, raia wa DR Congo, alitimuliwa kwenye timu hiyo Novemba, mwaka jana kutokana na kuonyesha kiwango kibovu katika michezo ya Ligi Kuu Bara kabla ya kuanza kudai fedha zake, hali iliyosababisha kuwafungulia kesi kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Zahera alisema kuwa amekuja nchini kwa ajili ya mchezo huo pamoja na kufuatilia madai ya fedha zake huku akiamini kuwa Yanga ina nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo.

 

“Nimekuja kuangalia mechi dhidi ya Simba lakini pia kufuatilia pesa zangu, nitakuwepo uwanjani kuangalia hiyo mechi siku ya Jumamosi maana kazi ilishapita hakuna shida.

 

“Naamini Yanga wanashinda kutokana na maboresho waliyofanya licha ya kwamba mchezo utakuwa ni wa nguvu kutokana na timu zote ambazo zitacheza kwa kukamiana ingawa Simba wanaonekana kukamia kwa kuwa wanaamini wana timu bora lakini kitakachowatokea hawataweza kuamini,” alisema Zahera.

SIMBA VS YANGA: MAZOEZI YA NIYONZIMA KWA MARA YA KWANZA AKITUA KAMBINI

Leave A Reply