The House of Favourite Newspapers

Zahera Awajaza Upepo Nyota Yanga

Mwinyi Zahera

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, ameweka wazi kuwa kasi ya kikosi chake na matokeo wanayoyapata ni kutokana na namna ya hamasa ya hali ya juu anayowapa wachezaji wake kabla ya mechi, kuhakikisha kwamba wanapambana na kuipatia timu hiyo matokeo mazuri.

 

Yanga wameendelea na wimbi lao la ushindi baada ya juzi Jumamosi kuwabutua Mbeya City kwa mabao 2-1 kwenye mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyopigwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

 

Baada ya ushindi huo, Yanga wamefikisha pointi 50 wakiwa vinara wa ligi hadi sasa wakiwa pointi 10 mbele ya wanaowafuatia Azam FC. Akizungumza na Championi Jumatatu, Zahera amesema kwamba matokeo wanayoyapata ni kutokana na hamasa kubwa ambayo anawapa kabla ya mechi na matokeo yake ndiyo yamekuwa yakizaa matunda na kupata ushindi.

 

“Ninawaomba wachezaji wangu wawe na morali ya juu na wapambane kwa kila hali kuona kwamba tunapata ushindi kwenye kila mechi na ndiyo maana tunapata ushindi hadi sasa,” alisema Zahera

STORI NA SAID ALLY

Comments are closed.