The House of Favourite Newspapers

Zahera Awapa Yanga Mil.60, Nyika Ajiuzulu

Kocha Mwinyi Zahera

AMSHAAMSHA ya Kocha Mwinyi Zahera ikichagizwa na Kamati ya Uhamasishaji ya Yanga, imekusanya shilingi 60,089,047. Zahera ndiye aliyeanzisha zoezi hilo la uchangishaji wa fedha zitakazotumika kwa ajili ya kusajili wachezaji watakaowatumia msimu ujao.

Mratibu wa timu hiyo, Hafi dh Saleh alisema fedha hizo wamezikusanya kupitia akaunti mbalimbali ikiwemo ya CRDB Benki ni Shilingi 54,594,079, M-Pesa 2,530,550 na TigoPesa ni 2,964, 418 pekee.

 

Mratibu huyo amewataka mashabiki wa timu hiyo kuongeza kasi ya kuichangia timu yao ili kufanikisha malengo ya kufi kia shilingi bilioni 1.5 anazozihitaji kocha kwa ajili ya usajili katika msimu ujao.

Katika hatua nyingine, Kaimu Mwenyekiti na Mjumbe wa Yanga, Samuel Luckumay na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Mashindano, Hussein Nyika, wamejiuzulu katika nafasi zao.

 

Luckumay alisema kuwa: “Lengo ni kupisha Uchaguzi Mkuu wa Yanga na kikubwa tumeona siyo vema kufanya uchaguzi mkuu wa nchi na klabu, mwakani katika kipindi kimoja.

 

“Niwahakikishie Wanayanga kuwa uchaguzi upo kama kawaida mwaka huu na hivi karibuni TFF kwa kushirikiana na Yanga wataanza mchakato upya wa uchukuaji wa fomu.”

 

Kwa upande wa Nyika, alisema: “Mimi nimejiuzulu nafasi zangu zote nilizokuwa nazo ndani ya Yanga, pia niwashukuru Wanayanga niliofanya nao kazi kwa pamoja kwa kipindi chote nilichokuwa naiongoza klabu hii.”

 

Yanga sasa itakuwa chini ya Baraza la Wadhamini linaloongozwa na George Mkuchika wakati mchakato wa uchaguzi mkuu ukiendelea.

STORI: WILBERT MOLANDI

Comments are closed.