The House of Favourite Newspapers

Zahera awatema Ajibu, Yondani Yanga SC

Ibrahim Ajibu (kushoto) akifanya yake.

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mkongoni, Mwinyi Zahera ameamua kuvunja ukimya baada ya kusema mchezaji yeyote ambaye anataka kuondoka ndani ya kikosi hicho ni ruksa.

 

Kwa sasa kumekuwa na tetesi za mastaa kibao wa timu hiyo wakihusishwa na timu nyingine kama Ibrahim Ajibu, Kelvin Yondani na Papy Kabamba Tshishimbi ambao wanaripotiwa kutakiwa na Simba.

 

Kutokana na tetesi hizo, Kocha Zahera alisema kuwa, haogopi kusikia mchezaji fulani anaondoka kwenye kikosi chake kwa sababu kuna wakati wachezaji hao ambao wanatajwa kuondoka wanakuwa hawapo kwenye timu na bado wamekuwa wakipata matokeo.

 

 

Kocha huyo alisema amekuwa akipigiwa simu na mashabiki ambao wamekuwa wakihoji kuwa wamekuwa wakisikia wachezaji Tshishimbi, Feisal Salum ‘Fei Toto’ na Yondani lakini yeye amekuwa akiwaambia wasijali mambo yatakwenda sawa hata kama wataondoka.

 

Zahera aliongeza kuwa tayari ameshawaambia viongozi wa timu hiyo kuwa hawapaswi kutetemeka wala kuwa na hofu kisa tu mchezaji fulani anaondoka klabuni hapo kwani kuna baadhi ya mechi wamekuwa wakishinda bila wao kucheza.

 

“Hakuna mchezaji yeyote anayeweza kuzuiwa kuondoka ndani ya Yanga na timu ikayumba hilo halipo na haliwezi kuniogopesha na mchezaji ambaye anataka kuondoka ndani ya klabu ruksa kwenda na Yanga itabaki kuwa bora.

 

“Nimejipanga kuhakikisha namaliza usajili wa wachezaji wangu mbele ya Mei 15, mwaka huu
kabla ya Juni Mosi ambapo itakuwa na majukumu ya timu ya taifa ya DR Congo huko Ulaya,” alisema Zahera.

Comments are closed.