The House of Favourite Newspapers

Zahera Kutua Nchini Julai 25, Kuelekea Siku Ya Mwananchi

Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera.

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, anatarajiwa kutua nchini Julai 25, mwaka huu kujiunga na timu hiyo katika maandalizi ya msimu ujao wa 2019/20.

 

Zahera ambaye kwa sasa yupo mapumziko baada ya kumaliza majukumu ya timu ya taifa akiwa kocha msaidizi wa DR Congo iliyoshiriki michuano ya Afcon nchini Misri, alitarajiwa kurudi mapema, lakini kwa sasa ameomba kuongezewa siku ili aweze kutatua matatizo ya kifamilia.

 

Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh, amesema kocha huyo atarudi Julai 25 kuendelea na maandalizi ambayo yameanza takribani wiki mbili sasa mkoani Morogoro.

 

“Kocha Zahera anatarajiwa kuingia nchini Julai 25, mwaka huu kuendelea na majukumu yake ya kukinoa kikosi chetu kuelekea msimu ujao.

 

“Amechelewa kutokana na kuomba kuongezewa siku za kuendelea kuwa mapumzikoni ili kuweka mambo sawa katika familia yake. “Lakini kipa wetu mpya, Farouk Shikalo, yeye muda wowote ndani ya wikiendi hii atakuwa amewasili,” alisema Saleh.

ONA QUEEN DARLEEN Alivyozua KIZAAZAA Jukwaani WASAFI FESTIVAL

Comments are closed.