iliadhimisha kwa kuwasaidia watoto hawa kwa kuwapatia vitu hivyo,huku kauli mbiu
ya mwaka huu ikiwa ni changia, okoa maisha.
hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society Bw. Francis Kiwanga
alisema kuwa wafanya kazi wa Taasisi hiyo huwa wanatenga asilimia moja kwa kila
mtumishi katika mshahara wake kwa ajili ya kurudisha fadhila na asante kwa jamii.
kusema kuwa wao kama waanzilishi wa kampeni hiyo walichanga na kufikisha million
sita, ila michango mingi ilitoka kwa wananchi na taasisi zilizoguswa na tatizo
hilo hivyo kuona haja ya kuwasaidia watoto hao.
mkurugenzi huyo alisema kuwa msaada huo utalenga watoto 100 waliopo katika camp
hizo kwa kufanyiwa upasuaji na mambo mengine madogo madogo yatakayohitajika
katika zoezi hilo.
taasisi ya Foundation For Civil Society ikishirikiana na wadau wake wameweza
kutoa kadi za bima ya afya za NHIF 100 ambazo zimegharimu kiasi cha zaidi ya shilingi
milioni 5 kuwasaidia watoto hao kwa matibabu hayo na mengineyo.
hawajiwezi na wanaohitaji michango yetu kwani kutoa ni moyo na kadiri unavyotoa
ndivyo unavyobadirikiwa.
wake Mkurugenzi wa kitengo cha mifupa MOI Dr. Respicious Boniface alisema kuwa
watoto hao wakipatiwa matibabu mapema wanaweza kuwa sawa kama watoto wengine,
lakini kinachofanya wazazi washindwe ni gharama za matibabu.
huyo alisema kuwa changamoto nyingine inayowakabili wao kama wauguzi ni uchache
wa vyumba vya upasuaji kwani vyumba vilivyopo havitoshi kwa kufanyia zoezi hilo ambapo amesema kuwa kwa siku wanawafanyia upasuaji zaidi ya wagonjwa 30.
huyo aliwapongeza shirika la Foundation for Civil Society kwa kuamua kuwasaidia
watoto hao ambao wanapata tabu kwa matatizo ya vichwa vikubwa na migongo wazi
na asilimia kubwa wazazi wao hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society Bw. Francis Kiwanga akizungumza katika maadhimisho ya Jumanne ya kutoa maarufu kama GIVING TUESDAY yaliyofanyika kitengo cha MOI Muhimbili Jijini Dar es salaam. |
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI Dr. Respicious Boniface akimkabidhi zawadi ya cheti Mwenyekiti wa UN chapter UDSM Bi. Faith Lawrance Katika shughuuli hiyo. |
Baadhi ya wazazi na wageni walioudhuria hafla hiyo ya kutolewa kwa msaada wa kusaidia matibabu kwa watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi jijini Dar es salaam. |