The House of Favourite Newspapers

Zaidi ya Watu 100 Wafariki kwa Joto Kali

0

WATU zaidi ya 100 wamekufa kutokana na kile kinachoelezwa kutokea hali ya ongezeko la kiwango cha joto katika kipindi hiki cha kiangazi katika maeneo kadhaa ya Canada na Marekani,hali imetajwa kuwa mbaya jimboni Oregon ambako kumetokea vifo 60 na Jimbo la Vancouver, British Columbia.

 

Polisi Canada kwa sasa inachunguza vifo 65 ambavyo vimetokea katika kipindi kifupi, baada ya kuanza fukuto la joto tangu Ijumaa iliyopita, pamoja na uchunguzi huo lakini idadi ya vifo bado inahofiwa uenda ikaongezeka.

 

Wimbi hilo la joto, ambalo katika baadhi ya maeneo limefikia nyuzi joto 45, watalaam wa hali ya hewa wanasema limetokana na mgandamizo wa hewa kutoka maeneo ya Kaskazini/mashariki na kiini chake kikiwa mabadiliko ya tabia nchi ambayo yalichochewa na shughuli za binadamu.

Leave A Reply