The House of Favourite Newspapers

Zama za Amber Lulu Kukaa Utupu Zimepita

MUUZA nyago ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva, Lulu Augen ‘Amber Lulu’ amefunguka kuwa, kipindi cha kukaa utupu ili mtu apate umaarufu kumepitwa na wakati.

Amber aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, hata yeye alikuwa akifanya kosa la kuacha mwili wake wazi, lakini sasa akili yake imepanuka na hataki kusikia mambo hayo.

“Kuachia wazi sehemu kubwa ya mwili kwa sasa ni ushamba na vitu hivyo vimepitwa na wakati. Hata mimi ninajilaumu sana,” alisema Amber Lulu ambaye awali alikuwa miongoni mwa mastaa waliojiachia utupu na kutupia picha mitandaoni.

Imelda Mtema | GPL

Comments are closed.