The House of Favourite Newspapers

Zamaradi Afunguka ‘Vita’ ya Nani Baba Halisi wa Patrick

MTANGAZAJI Zamaradi Mketema aliyepewa jukumu kuratibu msiba wa mtoto wa Muna, Patrick ametaka yeye asihusishwe juu ya mvutano uliopo kati anayedaiwa kuwa ni baba wa mtoto, Peter Zacharia na aliyekuwa mkewe Muna Love.

 

Hatua hiyo imekuja baada ya siku ya jana kusambaa taarifa mtandaoni kwamba yeye anachangia mgogoro huo kuendelea wakati Muna akisema msiba uko kwake Mbezi Beach na baba akisema msiba upo kwake Mwananyamala huku wakiacha maswali kuhusu baba halisi wa mtoto huyo iwapo ni Peter au Casto.

Akizungumza kwenye Exclusive Interview na Global TV Online jana nyumbani kwake Mwananyamala Darajani jijini Dar, Peter alisema Zamaradi amefanya jitihada kubwa za kuokoa uhai wa Peter na kuongeza kuwa licha ya mtoto huyo kufariki, amemwachia jukumu la kuzungumza na Muna ili wanaweza kuumaliza mgogoro wao ili mtoto azikwe kwa taratibu zote.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram, Zamaradi ameandika;

Stori kamili, picha na Video Install Global Pubishers App na uifungue

Android : =>  Play store

IOS : =>   APP store

“Naomba niongee, naona kuna sehemu naingizwa ambazo sidhani kama ninastahili kiukweli (mwenye akili ataona hilo). Huyu mtoto alinigusa sana kwenye ugonjwa wake na ndiomana nikaamua kufanya nilichofanya, na hakuna INFORMATION hata moja niliyoitoa bila kuwasiliana na mwenzetu (Muna) ambae ndie Mama Mzazi kila mtu anafahamu hilo.

“Na chochote nilichofanya nilifanya kwa moyo na roho nyeupe kwa kile ambacho kilionekana na wote kiubinaadamu, since kuna distractions na mambo yamekuwa yana migogoro ya kifamilia, nikiwa kama mtu baki NIMEAMUA KUHESHIMU na kuyaacha KWAO WAO WAYAMALIZE sababu WAO NDIO WANAJUA UKWELI.

 

“Nitashiriki maziko popote watakapoamua wao (kama watakaa na kukubaliana kifamilia) na sina neno lolote la kutia popote sababu sina ninachojua zaidi na wala sikuwa najua kama kuna kutokuelewana kokote nyuma ya pazia, hivyo tuheshimiane jamani.

 

“Kikubwa tuwaombee maelewano wafikie muafaka na mtoto alale anapostahili, na zaidi MUNGU awaongoze busara iweze kutumika ili Malaika huyu aweze kupumzika kwa amani. Asanteni.” ameandika Zamaradi.

 

VIDEO: Baba Halisi wa Patrick Afunguka Mazito, Kifo cha Mwanaye

Comments are closed.