The House of Favourite Newspapers

Zantel Yatoa Msaada Wa Saruji Na Mabati Kwa Waathirika Wa Mafuriko Wa Mkoa Wa Kusini Pemba

0

 

LW1
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kusini Pemba, Ndg. Yussuf Mohammed Ali (kushoto) akimtambulisha Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Bw. Mohamed Khamis Baucha (wa pili kushoto) kwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Mwanajuma Majid Abdallah (hayupo pichani) kabla ya Mkuu huyo wa Zantel kukabidhi msaada wa Saruji na Mabati kwa ajili ya waathirika wa mafuriko mkoani humo. Msaada huo una gharama ya Sh 13 milioni na lilifanyika jana kisiwani Pemba-Zanzibar. Wa tatu Kulia ni Ofisa wa fedha na Utawala wa Tawi la Zantel–Pemba, Yakoub Fadhil Juma.
LW2
Mkuu wa Kampuni ya mawasiliano ya Zantel-Zanzibar, Bw. Mohamed Khatib Baucha (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Mwanajuma Majid Abdallah mifuko ya Saruji kwa kwa ajili ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika mkoa huo. Zoezi la makabidhiano ya msaada huo lilifanyika jana mkoani humo ambapo Zantel walitoa jumla ya mabati 350 na Saruji mifuko 350, vyote vikigharimu Sh. 13 milioni.
LW3
Mkuu wa Kampuni ya mawasiliano ya Zantel-Zanzibar, Bw. Mohamed Khamis Baucha (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Mwanajuma Majid Abdallah mifuko ya Saruji kwa kwa ajili ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika mkoa huo. Zoezi la makabidhiano ya msaada huo lilifanyika jana mkoani humo ambapo Zantel walitoa jumla ya mabati 350 na Saruji mifuko 350, vyote vikigharimu Sh. 13 milioni. Kushoto ni Ofisa wa fedha na Utawala wa Tawi la Zantel–Pemba, Yakoub Fadhil Juma.
LW4
Mkuu wa Kampuni ya mawasiliano ya Zantel-Zanzibar, Bw. Mohamed Khamis Baucha (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Mwanajuma Majid Abdallah mabati kwa kwa ajili ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika mkoa huo. Zoezi la makabidhiano ya msaada huo lilifanyika jana kisiwani Pemba-Zanzibar ambapo Zantel walitoa jumla ya mabati 350 na Saruji mifuko 350, vyote vikigharimu Sh. 13 milioni
LW5
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Mwanajuma Majid Abdallah akizungumza na wakuu wa wilaya za mkoa huo Mhe. Salama Mbarouk Khatib wa wilaya ya ChakeChake (kushoto) na Hemed Suleiman Abdallah wa wilaya ya Mkoani( wa pili kushoto) kabla ya kuwakabidhi msaada wa Saruji na Mabati yaliyotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel kwa ajili ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika mkoa huo. Zoezi hilo lilifanyika jana kisiwani Pemba-Zanzibar ambapo jumla ya mabati 350 na Saruji mifuko 350 yalikabidhiwa na Kampuni ya Zantel.
LW6
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Mwanajuma Majid Abdallah akiwakabidhi wakuu wa wilaya za mkoa huo mabati yalitolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel kwa ajili ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika mkoa huo. Zoezi hilo lilifanyika jana kisiwani Pemba-Zanzibar ambapo jumla ya mabati 350 na Saruji mifuko 350 kwa pamoja vilikabidhiwa na Kampuni ya Zantel. (Katikati) ni Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mhe. Salama Mbarouk Khatib na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mkoani Mhe. Hemed Suleiman Abdallah.
Leave A Reply