The House of Favourite Newspapers

Zanzibar Yafutiwa Uanachama wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF)

0

Zanzibar imefutiwa uanachama wake katika Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ikiwa ni miezi minne tu imepita tangu walipokubaliwa na kuwa mjumbe wa shirikisho hilo.

Rais wa CAF, Ahmad Ahmad amesema kwa, Zanzibar ambayo ni sehemu ya Tanzania haikupaswa kabisa kukubaliwa kuwa mjumbe wa 55, uamuzi uliofanywa Machi 2017.

Rais huyo amesema kuwa, Zanzibar ilikubalia kuwa mwanachama wa CAF bila kuzingatiwa kwa vigezo vya msingi ambavyo ni muhimu, huku akifafanua zaidi kuwa, CAF haiwezi kuvikubalia vyama viwili vya soka kutoka nchi moja.

CAF imesema kuwa kigezo chao cha kutambua nchi ni ile inayotambuliwa na Umoja wa Afrika (AU) pamoja na Umoja wa Mataifa (UN).

Licha ya kuwa Rais wa CAF aliyepita, Issa Hayatou aliikubalia Zanzibar kuwa mwananchama, lakini Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) lilikataa kuifanya Zanzibar kuwa mwanachama.

Zanzibar ni sehemu ya Tanzania lakini kwenye masuala ya mpira imekuwa ikijitegemea. Katika mashindano ya kanda, imekuwa ikishiriki kama nchi.

Leave A Reply