The House of Favourite Newspapers

Zari Amchamba Mondi Laivu Bila Chenga

0

ZARI The Boss Lady; ni baby mama wa supastaa wa muziki barani Afrika, Diamond Platnumz anayeiwakilisha vyema Tanzania ambaye ametema nyongo kwa kumchapa jamaa huyo laivu bila chenga.

Ikumbukwe kwamba, Zari; raia wa Uganda anayeishi nchini Afrika Kusini amezaa watoto wawili na Diamond au Mondi ambao ni Tiffah Dangote na Prince Nillan.

 

Katika sehemu ya pili ya shoo yao ya Young, Famous and African inayoendelea kwenye jukwaa la Netflix katika Mtandao wa YouTube, Zari anapiga stori na mwigizaji Khanyi Mbau wa Afrika Kusini ambapo anamueleza kwamba aliona ni bora alee watoto wake mwenyewe kuliko kuwa na kinyongo na Diamond ambaye alimsaliti mara nyingi mno.

 

Mwishoni mwa sehemu hiyo ya pili ya shoo hiyo ndipo hapo Zari akawa uso kwa uso na Diamond ambapo anamchamba laivu akifunguka yote mazito ambayo hajawahi kufunguka.

 

Zari anamwambia Diamond hivi aliwahi kuwaza kuwa na familia yake; kwa maana awe na Zari kama mke hapa na watoto wake hapa?

Hapo Diamond hakuwa na majibu na kumfanya Zari kuendelea kumpa somo kwamba alimkatia tama na kumfanya jamaa huyo atulie tuli!

 

Zari anamwambia Diamond: “Unaona ulivyojishusha kama hapa, hukuwahi kujishusha wakati ule tukiwa pamoja, ulikuwa unapanda juu sana, ulijiona staa mkubwa, lakini nadhani leo umeelewa ni hasara kiasi gani umesababisha.”
Zari anaendelea; “Nilikuwa na uwezo wa kupigwa risasi kwa sababu yako kwa jinsi ambavyo nilikuwa ninakupenda.
“Mimi na watoto tulikuwa tunashambuliwa Baba Tee (Diamond), tulikuwa tumechoka, hukutulinda, hukufanya chochote.”

 

Wakati wote huo Zari akiwa anafoka kwa hisia kali na kulengwalengwa na machozi, Diamond alikuwa anatazama pembeni na kujigeuza asijue nini cha kujibu kwa namna alivyomuumiza kutokana na usaliti aliomfanyia kiasi cha kuzaa nje ya uhusiano wake ambapo alizaa na Hamisa Mobeto.

 

Itoshe kusema kuwa, kwenye shoo hii, hasa sehemu hii ya pili, Zari amemtolea uvivu Diamond na kutoa kile kilichoukamata moyo wake juu ya mzazi mwenzake huyo, jambo ambalo hakupata kulifanya.
Kwa kufanya hivyo, wengi wanaamini kuwa, Zari atakuwa ametoa kitu kikubwa na sasa roho yake itakuwa kwatu kabisa.

STEVE NYERERE ALIPUKA – “NILIKATAA KUWA MSEMAJI WA MZIKI, WAKANILAZIMISHA SANA, SIJAWAHI KUOMBA”

Leave A Reply