The House of Favourite Newspapers

Zari Ashtua Mamilioni ya Wafuasi Wake

0

MIONGONI mwa stori zilizotrendi wikiendi iliyopita ni pamoja na kitendo cha mwanamama tajiri, Zarinah Hassan almaarufu Zari The Boss Lady, kutoposti chochote kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kiasi cha kushtua wafuasi wake ambao ni mamilioni.

 

Zari ambaye ni baby mama wa staa wa muziki barani Afrika, Nasibu Abdul au Diamond Platnumz ambaye amezaa naye watoto wawili, Tiffah Dangote na Prince Nillan, hadi jana Jumapili alikuwa zaidi ya wiki moja bila kuposti chochote, jambo ambalo linaibua maswali kwa wafuasi wake hao ambao wanasema kuwa, hawajamzoea hivyo.

Mara ya mwisho kwa Zari kuposti kwenye ukurasa wake wa Instagram ilikuwa Agosti 21, 2021 ambapo aliposti picha yake akiwa na mwanaume aliyemtaja kama kaka yake ambaye ilikuwa ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya mwanaume huyo.Baada ya kuposti picha hiyo, Zaria aliandika; “Happy birthday my beloved kaka. You are one of a kind and a blessing to have. I love you bro, always and forever @adamzdee7.”

 


Baada ya siku hiyo, Zari
hakuonekana tena akiposti chochote hata kwenye kurasa za watoto wake za Princess Tiffah na Prince Nillan ambazo yeye ndiye huzisimamia.

 

Hata hivyo, baada ya maswali kuwa mengi, alianza kuposti vipande vya video kwenye Insta Story hivyo kushusha kidogo presha za wafuasi hao.

 

Ukiacha mitandao mingine ya kijamii kama TikTok na Snapchat, kwenye ukurasa wake wa Instagram pekee, Zari ana zaidi ya wafuasi milioni 9.5

STORI; MWANDISHI WETU – GPL

Leave A Reply