The House of Favourite Newspapers

Zari, Wema Ni Piga Nikupige

0

NI piga nikupige! Hicho ndicho kinachojiri baina ya maeksi wa supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na Wema Isaac Sepetu.

 

Kwa takriban wiki nzima sasa moto umewaka kati ya Wema na Zari ambapo mmoja akitupa jiwe, mwingine anajibu mapigo.

 

Bifu hilo jipya limeibuka baada YA Wema kujibu kijembe cha Zari alichokirusha yapata miezi miwili iliyopita, kipindi kile mbwa wake aitwaye Manunu alipopotea.

 

Wakati ule, mmoja wa wafuasi wa Zari alimuuliza mwanamama huyo kama amemuona Manunu wa Wema ambapo mama huyo wa watoto watano alijibu kuwa mbwa huyo hakupotea bali alikuwa anatafutiwa kiki.

Vyanzo vya ndani vinasema kwamba, wakati Wema akijiandaa kumjibu Zari ndipo Taifa la Tanzania likapatwa na msiba mzito wa Hayari Dk John Pombe Magufui hivyo haikuwa busara kuendelea na majibizano.

 

Hata hivyo, wikiendi iliyopita Wema alitumia vizuri nafasi ya vipaza sauti na kamera za waandishi alipohudhuria kwenye uzinduzi wa tamthiliya.Katika majibu yake, Wema aliwataka wafuasi wake kumpuuza Zari kwa kuwa ni muongo.

 

Kwa upande wake Zari, aliposikia majibu hayo ya Wema naye alijibu mapigo kwa kumtaka kula kwanza chakula kwani amebaki kcihwa tu.

 

Jambo hilo halikumfurahisha Wema ambaye naye alitumia kurasa zake za mitandao ya kijamii akisema kuwa akiendelea kubishana na Zari ni kumkosea heshima mtu mzima na kujitafutia laana.

“Kugombana na watu wazima ni kujitafutia laana…na mimi nina heshima sana kwa wakubwa wangu…pia ni msikivu…nafanyia kazi mashauri…”

 

Alijibu Wema.Kwa kiasi f’lani, wafuasi wake walidai kuwa ameshinda vita, bila kujua Zari ameandaa bomu gani kwani huwa hapendi kuitwa mtu mzima.Kupitia kwa mmoja wa mashabiki kidakindaki, Team Zari wamejibu; “Zari kwani wewe ni mtu mzima? Kwani mtu mzima huwa yupo vipi?

 

Ninavyojua mtu mzima ni yule ambaye yupo juu ya umri wa miaka 18.”Kwa upande wake Zari naye akajibu; “Wanajiona wasichana bado wakati umri umeenda bila mafanikio na wamebakisha vichwa tu kama maboflo.

 

Bifu la Zari na Wema lilianza muda mrefu baada ya Wema kumtuhumu Zari kwamba ndiye aliyemchukuliwa mpenzi wake, Mondi kipindi kile.Tangu hapo, Wema na Zari hawakuwahi kupikika chungu kimoja kwani hata wakati Zari anaachana na Mondi mwaka 2018, Wema alitajwa kuwa chanzo cha yote.

Stori; Mwandishi Wetu, Dar

Leave A Reply