The House of Favourite Newspapers

Zawadi Wanazozitoa Infinix Kwa Wateja Wao

0

Msimu wa sikukuu ni kipindi ambacho watanzania na watu wa mataifa mbalimbali hupenda kufanya manunuzi makubwa bila kusahau zawadi kwa wawapendao, rafiki, ndugu, watoto, wazazi.

 

Kupitia mazoea haya, kampuni ya Simu, Infinix Mobile Tanzania, inayofahamika kwa simu zenye uwezo mkubwa wa Camera na Battery imewaandalia wateja wake zawadi mbalimbali kupitia promosheni yao inayokwenda kwa jina la DECEMBER TO REMEMBER, KISHUASHUA.

 

Ofa inakwenda hivi, kwa kila mteja atakayenunua toleo jipya la Infinix S5 mojakwamoja atakuwaameingia katika droo ya kushindania zawadi kemkem kama vile Vacuum Cleaner, Deep fryer, Subwoofer Radio, shopping voucher, Movie Ticket na Coupon kwaajili ya kupata msosi katika restaurant za kibabe na zawadi nyingine kutolewa papohapo.

Droo kubwa kuchezeshwa kila Jumamosi katika duka lao la kisasa Infinix Smart hub Mlimani City na Ofa hii ni kwa msimu wote huu wasikukuu.

 

Chakufanya fika sasa katika maduka yao yenye promotion jijini Dar ES Salaam na ujipatie simu ya kijanja Infinix S5 yenyekamera 5 upate zawadi kwajiliyako na familia yako.

 

 

 

 

Leave A Reply