Mastaa Hawa Wamezidi Kutoboa Kimataifa 2019

 

KOLABO za kimataifa na wasanii wakubwa ambao wanajulikana kwenye anga la muziki kimataifa, mara nyingi huwa zinamsogeza mbele msanii na muziki kwa jumla.

Katika kufunga mwaka 2019, IJUMAA SHOWBIZ inakuletea kolabo za wasanii Bongo Fleva ambazo zimezidi kuusogeza mbele muziki huo kwa mwaka huu;

 

RAYVANNY

Kwa mwaka huu Rayvanny anatajwa kuwa kinara wa kolabo za nje. Kolabo hizo zimeweza kufika mbali kutokana na watu aliofanya nao kwa kuwa ni wakubwa kimuziki duniani.

 

Kolabo hizo ni pamoja na Tetema Remix ya kwanza aliyoifanya na wasanii wakubwa ambao ni PitBull, Mohombi na JayOn, wote wakiwa wanatokea nchini Marekani.

Kolabo ya pili ya kimataifa ni Tetema Remix namba mbili ambayo aliifanya na wasanii wawili wakubwa kutoka Nigeria, Patoranking na Zlatan Ibile.

 

Ukiachana na kolabo hizo, pia Rayvanny aliachia kolabo mbili kali na zote akiwashirikisha wasanii wakubwa kutoka Nigeria ambao ni Mayorkun ambaye alifanya naye ngoma inaitwa Gimme Dat na nyingine ni ngoma inaitwa Slow ambayo amefanya na mkali anayeitwa Phyno.

Nyingine ni Mmmh aliyofanya na Willy Paul wa Kenya na Pepeta aliyofanya na Nora Fatehi mwenye asili ya Canada.

 

HARMONIZE

Mkali anayemiliki lebo ya muziki ya Konde Music Worldwide naye ndani ya mwaka huu, ameweza kupiga kolabo kibao kubwa ambazo zimeweza kufika mbali kimataifa. Kolabo ya kwanza ni ile ya Kainama ambayo amefanya na wakali akiwemo Burna Boy wa Nigeria na aliyekuwa bosi wake pale WCB, Diamond Platnumz.

 

Kolabo iliyofuatia ni ile aliyomshirikisha mwanadada Yemi Alade wa Nigeria inayokwenda kwa jina la Show Me What You Got. Ukiachana na hizo, kuna nyingine ambazo ni Oyoyo akiwa na Skales wa Nigeria na Guondo Sakit ambayo aliimba na msanii wa Sudan aitwaye John Frog. Nyingine iliyobamba ni ile ya Inabana akiwa na Eddy Kenzo wa Uganda.

 

BEN POL

Mkali huyu wa RnB Bongo, mwaka huu miezi kama minne iliyopita alifanya maajabu baada ya kuachia ngoma aliyoipa jina la Sana akimshirikisha Timaya wa Nigeria. Nyingine ni Mmoja aliyofanya na Naiboi wa Kenya.

 

DIAMOND

Diamond au Mondi ana kazi nyingi sana ambazo zimevuka kimataifa, lakini kolabo za kimataifa ndizo ambazo zimeweza kumjengea sifa za kuingia kwenye orodha ya wasanii kumi bora barani Afrika.

Kolabo hizo alizofanya Mondi ni Yope Remix aliyofanya na Inno’s B wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

 

Mbali na hiyo, Mondi alitisha baada ya kuachia ngoma iliyowateka wanasoka wakubwa duniani, Paul Pogba wa Manchester United na Didier Drogba wa Ivory Coast. Ngoma hiyo ilikwenda kwa jina la Inama akiwa na Fally Ipupa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Nyingine ni Moto aliyofanya na Wawa Salegy wa Madagascar na Sound aliyofanya na Teni wa Nigeria huku ile ya kwake na Wizkid ikiwa jikoni.

 

JUX

Mwaka huu umekuwa wa mafanikio makubwa kwake kwani alifanikiwa kuachia albam yake ya The Love.

 

Jux amefanya kolabo kadhaa ambazo zimemfanya akae kwenye ramani ya muziki wa kimataifa zaidi kwa mwaka huu. Kolabo hizo ni pamoja na ile Incase You Dont Know akiwa na Nyashinski wa Kenya. Pia ana ngoma nyingine ya Fashion Killer aliyoshirikiana Singah wa Nigeria.

 

V-MONEY

Nje ya boksi V-Money amepambana kadiri awezavyo ili kuufikisha muziki wake mbali. Mwaka huu V-Money alifanya kolabo kubwa ambazo zimefika mbali kiasi cha kuchezwa kwenye moja ya mechi kubwa ya mpira wa kikapu nchini Marekani.

 

Kolabo hizo ni pamoja na Bambino ambayo ameshi-rikiana na Reekado Banks wa Nigeria. Pia aliachia ngoma akiwa na Kundi la Distruction Boyz la Afrika Kusini iliyokw-enda kwa jina la Thats for Me. Alifanya Never Ever Remix akiwa na wanamuziki maarufu duniani; Frederic Gassita wa Gabon na The London Symphony Orchestra wa Uingereza.

 

MBOSSO

Jamaa aliweka rekodi rekodi kwa kupiga kolabo ya Ngoma ya Shilingi akimshirikisha Reekado Banks wa Nigeria.

 

 

Toa comment